Leo ni ile siku iliyosubiriwa sana hatimaye hayawihayawi sasa yamekuwa katika mochuano ya raundi ya kwanza katika ligi ya mabingwa Afrika.
Leo kitapigwa kipute kati ya ASAS Djibouti FC ya Djibouti na Young Africans ya Tanzania katika uwanja wa Chamazi Complex, Dar es salaam unaomilikiwa na Azam Football club matajiri hawa wa jiji.
Mechi hiyo itachezwa leo katika uwanja huo wa chamazi complex majira ya jioni saa 11:00 ikiwa ni mzunguko wa kwanza ambapo ASAS Djibouti FC ndio wapo nyumbani wakitumia dimba la Chamazi Complex kama uwanja wa nyumbani wakiikaribisha timu ya wananchi Young Africans.
Mchezo huo utarushwa live na kituo cha television cha Azam ambapo itawapa watu fursa ya kushuhidia mechi hiyo popote Duniani.
Shukrani kwa waandaaji wa mashindano haya ya CAF Champions league yanayodhaminiwa na Total Energies kama mdhamini mkuu na 1XBet kama mdhamini mwenza.
Tukutane Chamazi Complex saa 11 kamili jioni leo siku ya jumapili ya tarehe 20 Agosti, 2023.
Comments
Post a Comment