Mchezo wa kwanza wa mashindano ya ngao ya jamii utakaochezwa leo tarehe 9 mwezi Agosti 2023 utachezwa kati ya miamba miwili ya Dar es salaam yaani Dar es salaam Young Africans maarufu kama Yanga na matajiri wa jiji la Dar es salaam Azam FC vijana hawa wa chamazi wana lambalamba au waoka mikate.
Mchezo huo utapigwa leo majira ya saa moja kamili usiku mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwakwani ambapo ndio mahali itakapochezwa michezo yote ya ngao ya jamii.
Pia mechi kati ya Simba na Singida Fountain gate utachezwa siku ya kesho tarehe 10 Agosti uwanja huohuo wa mkwakwani Tanga.Wananchi na mashabiki wa mpira nchini wana shauku kubwa ya kushuhudia mashindano hayo ambayp ni mwanzo wa ufunguzi wa msimu mpya ya ligi kuu ya NBC baada ya kukaa kwa kipindi kirefu bila kuwepo kwa machindano au mechi za ligi kuu.
Sasa furaha ya mashabiki wa mpira wa miguu itarejea na burudani kupatikana kwa wingi na hivyo wadau wote wa mpira wajiweke tayari kwa msimu huu mwengine wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara.
Comments
Post a Comment