Simba na Yanga Kukipiga Leo

 

Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu sana na mashabiki wa mpira wa mguu ambao pia ni mashabiki wa timu pendwa za Simba na Yanga imefika.

Hii ni baada ya nusu fainali ya Yanga na Azam kuchezwa na kupatikana mshindi ambae ni Yanga alieshinda kwa goli 2 kwa sifuri na pia wekundu wa msimbazi Simba kukipiga na Singinda Fountain Gate ambapo walitoka sare ya bila kufungana magoli iliyopelekea mikwaju ya penati ambapo mnyama aliibuka kidedea na kutinga fainali na kumfuata mtani Young Africans.

Fainali hii ya ngao ya jamii ambayo pia ni mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara itachezwa leo katika dimba la mkwakwani Tanga. Fainali hii ni kati ya Simba na Yanga ambapo leo lazima mshindi apatikane ile ndani ya dakika tisini au kwa mikwaju ya penati na kisha kubeba taji hilo la ngao ya jamii.

Mechi hiyo itachezwa leo siku ya jumapili majira ya saa 1:00 usiku katika mkoa wa Tanga katika uwanja wa mkwakwani na kurushwa live au mubashara na kituo cha televisheni cha Azam TV.

Comments