Simba na Yanga Waweka historia Klabu Bingwa Afrika

Watani wa jadi Simba na Yanga kwa pamoja wamefanikiwa kwa pamoja kutinga katika hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika.


Timu hizi mbili ambazo ni timu pendwa zaidi na mashabiki wa mpira wa miguu Tanzania, zimepiga hatua hii muhimu kwa pamoja jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya mpira wa miguu hapa nchini.


Kufanikiwa kwa timu hizo kunatokana na Yanga kushinda kwa magoli ya jumla 3-0  dhidi ya Al Merekh ya Sudani, na Simba ikipita kwa matokeo ya jumla ya 3-3 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia huku Simba ikipita kwa kanuni ya goli la ugenini.

Mafanikio ya timu hizo mbili kubwa zaidi Tanzania  kunaifanya Ligi Kuu Tanzania kuzidi kung'ara zaidi na kuupaisha mpira wa Tanzania anga za kimataifa.

Comments